Friday, 27 May 2016

Huu Udhalilishaji wa huyu Harmonizer Kusema Sepetu Katoa Mimba inaweza kumpeleka Jela Harmonize

WEMA2Wema Isaac Sepetu ‘Madam’

Dar es Salaam: Endapo mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ atalivalia njuga suala la kudhalilishwa mtandaoni na msanii aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, jamaa huyo atakwenda jela miaka kadhaa na faini juu.
harmonize kasuku - bekaboyRajab Abdulhan ‘Harmonize’
CHANZO NI NINI?
Juzikati, Harmonize au Hamo, akiwa na kundi la wasanii wenzake katika eneo ambalo halikujulikana ni wapi, walijichukua clip (kipande cha video) kwa staili ya kujipiga ‘selfie’ huku Harmonize akiimba wimbo wa msanii Stamina uitwao Mwambie Mwenzio, ambao kwenye mistari hiyo dogo huyo alisherehesha kwa kusema kuwa, usitoe mimba usije ukaja kulia kama (Wema) Sepetu.
HARMONIZE ALA ZA USO
Baada ya Harmonize kuwaongoza vijana hao kumdhalilisha Wema kwa staili hiyo, watu wengi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii walimpa jamaa huyo za uso, baadhi wakisema kuwa, umaarufu mdogo alioupata unamzuzua.
Wema SepetuWema na mama yake mzazi.
“Huyu mtoto anaona ameshakuwa maarufu sasa, anaona sawa kuwatukana hata wakubwa zake au ametumwa?” alihoji mmoja wa mashabiki wa Wema (Team Wema) aliyejitambulisha kwa jina la C_K kwenye Mtandao wa Instagram.
Mwingine akaandika: “Ninachojua huyu dogo anatafuta kiki lakini siyo kwa kufanya mambo haya, hivi ana ushahidi gani kama Wema katoa mimba?”
Harmonizer-na-WolperHarmonize na Wolper
KAULI YA TCRA
Akizungumzia sakata hilo, Afisa kutoka Dawati la Malalamiko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Doris Mhimbira alisema kuwa ni kosa la jinai ambalo mlalamikaji akiwa ‘serious’ anaweza kusababisha Harmonize akachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema kitendo alichokifanya Harmonize, endapo Wema atakwenda kulalamika na uzuri ni kwamba jina la mlalamikiwa linajulikana hivyo sheria itachukua mkondo wake. (Kwa mujibu wa sheria ya mtandao anaweza kwenda jela kati ya mwaka mmoja hadi saba na faini juu.)
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana ni kwamba Wema hajalikalia kimya suala hilo kwani anadaiwa kawasiliana na wanasheria wake ili kumfunga jamaa huyo.
MAMA WEMA SASA
Hata hivyo, wakati kila kona yakirushwa makombora kuelekezwa kwa Harmonize na timu yake (Team Harmonize), yakavuja madai kuwa, mama wa Wema, Mariam Sepetu aliona clip hiyo na kwamba alikwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ili kushinikiza kijana huyo kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.
WEMA AJIBU KIAINA
Baada ya Wema kuona clip hiyo alionekana kuumizwa na maneno hayo, akaamua kutupia picha mtandaoni akiwa na mama yake kisha akaandika; ‘Ipo siku na mimi nitaitwa mama’.
HARMONIZE ATAFUTWA!
Kufuatia ishu hiyo kuwa gumzo mjini huku kila mmoja akimlaumu Harmonize, Ijumaa lilimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopatikana alisema, anashangaa watu kumjia juu kwa kuwa yeye hakumtaja Wema kwenye clip hiyo ila jina lililotajwa ni Sepetu.
“Tuachane na hayo mambo bwana, mimi sijamtaja Wema pale, jina lililotajwa ni Sepetu sasa Wema na Sepetu wapi na wapi?” alijitetea Harmonize.
SEPETU GANI?
Alipobanwa kuwa ni Sepetu gani ambaye walikuwa wakimlenga ambaye ametoa mimba, hakujibu badala yake alikata mawasiliano.
IJUMAA LAMTAFUTA MAMA WEMA
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta mama Wema ili kujua aliichukuliaje clip hiyo na kama ni kweli alikwenda polisi, hata hivyo simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
WEMA HUYU HAPA
Baada ya mama Wema kukosekana, Ijumaa lilipata fursa ya kuwasiliana na Wema ambaye katika hali ya kuonesha kutofurahishwa na kitendo hicho, alimbutua Harmonize kwa kusema kuwa hajitambui ndiyo maana anafanya mambo ya kitoto.
“Kwanza nipo bize sana na kazi, hao ni watoto wadogo hao hawajielewi,” alisema Wema.
Alipoulizwa kwamba huenda ni mpango wa kumtibulia mchongo wake anaoupigia kampeni wa Wema App, mwanadada huyo alisema kama ni hivyo yeye na walio nyuma yake siyo wasomi na bora kuachana nao.
Hata hivyo, taarifa zilizovunjwa ni kwamba, Harmonize anafanya kila awezalo ili kumpa mimba mpenzi wake wa sasa, mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.
Harmonize alipoulizwa kuhusu hilo alisema kuwa, hiyo ni mipango ya Mungu na ikitokea itakuwa mwake tu.
TUJIKUMBUSHE
Katika mambo ambayo yamekuwa yakimuumiza Wema ni pamoja na watu kumuita mgumba sambamba na kumpa skendo ya kutoa mimba kila anaponasa.
Katika siku za hivi karibuni, Wema alinasa mimba lakini inavyonekana haikuwa riziki kwani miezi kadhaa baadaye ilidaiwa kuchopoka.