Wednesday, 13 July 2016

NAFASI YA BABA KATIKA MALEZI NA MAENDELEO YA MTOTO !!

Kama ni kweli kuwa mtoto hawezi kuzaliwa bila ya baba na mama basi hawezi kukamilika bila ya baba na mama. Ni kweli tumesikia na kujifunza mengi kuhusu mama na nafasi yake kwa mtoto. Mama anao wajibu wake kama mama na ndio maana ni mama na hawezi kuwa baba. Mama anaweza kuyafanya mambo mengi kama baba lakini hawezi kuwa na ladha ya baba. Hivyo basi nafasi ya baba ni muhimu kwa malezi na makuzi ya mtoto. 
Na nafasi ya baba na umuhimu wake ni zaidi ya pesa anazotoa kwa matumizi ya familia na huduma kwa mtoto. Baba anayo nafasi kubwa sana kwa mtoto katika kukua kwake na hata maendeleo yake. Malezi na maendeleo ya mtoto aliyekosa baba huwa na mapungufu kwa mtoto kijamii,kisaikolojia,kibaolojia,kiakili, kiroho na hata kimaumbile.

kumbeba mtoto humjengea mtoto uwezo wa kujua wewe kama mzazi unaupendo kwake.
Bila baba maisha ya mtoto hukosa mengi ambaye humfanya mtoto kutokamilika. Mtoto bila baba hatakamilika hata awe na umri mkubwa kivipi. Na ikumbukwe kuwa sio kila mtu anayeonekana ni mtu mzima amekamilika kimakuzi na muda mwingine wengine hushindwa kuwa baba kwasababu hawakupata malezi ya baba, hivyo hawakukamilika. Baba ni ukamilifu wa mtoto. Kama mtoto hawezi kuzaliwa bila baba na mama basi hawezi kukamilika bila malezi ya baba na mama. Mtoto anamhitaji baba. Mwanaume anapokuwa baba dunia yake hubadilika, na yeye huwa zaidi ya mume wa mtu – kwasababu – anaingia katika wajibu wa kulea na kumwongoza mtoto.
Na katika familia wababa wengi huonekana kimwili zaidi, lakini moyoni wengi wao huwa hawapo - kwani wengi huwa mbali na watoto kiasi ambacho huonekana kama wasaidizi tu katika kumlea mtoto na kujisahau kuwa , mama hawezi kuwa badala ya baba na wao kama wakina baba wanao wajibu mkubwa zaidi, mbali na kuhudumia familia , pia wanahusika sana katika makuzi ya watoto wao kama wababa.
Baba ni ufunguo wa mtoto kupata ujasiri wa maisha, sio kwamba mama hawezi kuyafanya hivyo bali mama hufanya kwa nafasi yake, lakini ladha ya kibaba inapatikana kwa baba mwenyewe. Baba anahusika sana katika malezi na makuzi ya mtoto , hasa katika mambo yafuatayo;
a) Baba ni Nguzo ya Kujenga Mahusiano Mazuri na Mama wa watoto: Kipimo kikubwa cha ubaba si uwezo wa kifedha tu peke yake, si umbile na wala sauti yake bali ni uwezo wa kutengeneza mfumo mzuri wa mahusiano kati ya yeye na mke wake. Baba ni kichwa cha familia, ni mhusika mkuu anayetakiwa kutengeneza mfumo wa familia. Ni mhusika mkuu anayetakiwa kujenga nguzo za ndoa kama amani,upendo,maendeleo na uwajibikaji. Ndoa ina mengi lakini ni baba ndio mwenye mengi ya kuifanya ndoa ikae sawa. Kwa kuyafanya hayo huweza kujenga picha nzuri kwa watoto na hata katika kukua kwao.
b) Kuwa na muda mzuri na watoto: Akili ya mtoto mdogo hutafisiri na hutambua mapenzi kwa muda mtu anaochukiwa kuwa na mtoto huyo. Kwa bahati mbaya katika jamii yetu muda wa baba katika familia huwa ni mchache sana; hata kama dunia ipo busy kiasi gani baba anatakiwa kujua kuwa muda wake na familia ni wa maana sana katika maisha ya watoto. Watoto huweza kujifunza mengi sana kwa uwepo wake na baba pia anaweza kuyajua mengi ya watoto wake na hata kuyarekebisha au kuyaboresha.
c) Baba ni mlinzi na mhusika mkuu wa Familia:
 Baba ni kiungo muhimu katika familia, ni mhusika mkuu katika kuhudumia familia na hata ulinzi wa watoto. Kipimo cha mwanaume si uwezo wake wa kimwili bali ni uwezo wa kutoa huduma katika familia na hata kuwa mhusika mlinzi wa watoto katika usalama wao kimaadili na hata kitabia. Hata kama baba hana uwezo wa kifedha bado anayo nguvu ya kibaba katika hili. Si kwamba mama hawezi kuwalinda watoto,lakini hawezi kufanya kama baba, yatupasa wote tufahamu ya kuwa; hakuna mama kama baba na wala hakuna baba kama mama.
d) Baba ni mwalimu wa familia:
 Maisha yana mengi ya kujifunza, mtoto ni kiumbe asiye na kosa. Hupokea na kujifunza chochote atakachofundishwa. Ni wajibu wa baba kujua mtoto ajifunze nini katika maisha, ajue nini na aishi vipi. Baba amepitia mengi na katika hayo baba anaweza kuzungumza na mtoto katika lugha ya kawaida ili kumfunza mtoto katika hayo. Baba ni mwalimu wa maisha kwa mtoto. Baba ni zaidi ya kocha wa mpira katika maisha ya mtoto. Baba ni dunia ya mtoto.Hatima ya maisha ya mtoto katika makuzi,maisha,nidhamu na hata maadili ipo mikononi mwa baba. Baba ni mhusika mkuu na kisababishi kikubwa cha kwanini mtoto awe/ amekuwa jinsi alivyo. Baba ni ufunguo wa maisha ya mtoto.
e) Baba ni mfano wa kuigwa wa mtoto (role model) :
 Uhusiano wa baba na mtoto una maana kubwa sana. Baba ni chanzo cha kwanini mtoto hufeli au hufaulu , chanzo cha mtoto kujua au kutokujua. Maisha ya baba ni picha ya maisha ya baadaye ya mtoto. Tabia ya baba ya nje na ndani ya familia ni kioo cha mtoto. Yawapasa wakinana baba wote watambue kuwa: ‘Wao ni kioo cha familia, haswa kwa watoto’. Chochote kile anachofanya nje na ndani ya familia,vyovyote vile anavyoishi na watu wa nje na ndani ya familia na hata matumizi ya hela na kazi yake ndivyo anavyomjenga au kumbomoa mtoto.

Nahitimisha kwa kusema; kuwa baba si kuzaa tu , maana ingekuwa hivyo - hata wanyama wanazaa pia. Kuwa baba ni zaidi ya kuzaa; ni kuwa mhusika kwa kujua kabisa kuwa maisha ya mtoto yanaweza kutengenezwa au kuharibiwa kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa mwongozo kutoka kwa baba. Hivyo basi baba anayo nafasi kubwa sana katika malezi na maendeleo ya mtoto katika maisha yake, mtoto ambaye ndiye anayetegemewa kuijenga nchi yetu ya Tanzania.
Simameni basi wakina baba na mchukue nafasi zenu, wako wapi wakina baba ambao watasimama na mimi leo na kusema, tutashiriki kikamilifu katika malezi na makuzi, pia katika kulinda familia zetu na kuongoza watoto wetu kwa hekima, busara na upendo?
Tuwapende na kuwalinda watoto wetu.
SMGEO

Sunday, 10 July 2016

Kutana na Mtanzania aliyetengeneza gari la kifahari kwa miezi mitatu !!

Picha za gari aina ya Kaparata lililotengenezwa na Mtanzania kutoka Gongo la Mboto, Dar es Salaam

 0
Gari aina ya Kaparata lililobuniwa na kijana mtanzania kutoka Gongo la Mboto Dar es Slaam Jacob Louis Kaparata (38).
Akizungumza wakati wa maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kaparata ameeleza kuwa alitumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchi kuunda gari hilo na kuwa miongoni mwa vitu hivyo vingine alivitengeneza mwenyewe na vingine alichukua vya aina nyingine ya magari.
Chassis nimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi nimelisuka kwa kutumia brake pipes zinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayo yanatumika kutengenezea mageti,” alisema Kaparata.
Injini, diff, gear box na matairi, vyote ni vya gari aina ya Suzuki Carry. Na nimelitengeneza kwa muda wa miezi mitatu na limenigharimu kiasi cha TZS 12,850,000.
 Kijana Jacob Louis ‘Kaparata’ (38) akimwelekeza mmiliki wa blogu ya Taifa Kwanza! jinsi alivyolitengeneza gari lake la kifahari aina ya ‘Kaparata’ kwa kipindi cha miezi mitatu tu.
Jacob Louis ‘Kaparata’ akiingia kwenye gari lake alilolitengeneza mwenyewe kwa miezi mitatu.
Wananchi wakipigana vikumbo kulishangaa gari la ‘Kaparata’ katika viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa amekutana na changamoto nyingi kwenye kutengeneza gari hilo hasa suala la ufundi ambapo mara nyingine alikuwa akipeleka bati au bomba likunjwe kwa vipimo alivyotaka yeye lakini fundi anakosea hivyo inamlazimu kutupa na kuanza upya.
Changamoto nyingine ilikuwa ni kukatishwa tamaa ambapo watu walikuwa wakimwambia kuwa hawezi na kuwa suala la kutengeneza magari awaachie wazungu.
Mbali na ugunduzi huu wa kuvutia, Kaparata anafanya kazi SIDO Vingunguti ambapo anatengeneza mashine za kutotole vifaranga. Na alisema kuwa akiamua kutengeneza gari jingine, ndani ya mwezi mmoja atakuwa amekamilisha.

(3015)
Views

Jacob Louis akiingia kwenye gari lake kuliwasha kuonyesha kwamba linafanya kazi barabara.
KWA Jacob Louis ‘Kaparata’ (38) mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kutokusoma shule hakujamzuia kuonyesha kipaji chake cha ubunifu baada ya kufanikiwa kutengeneza gari la kifahari aina ya ‘Kaparata’ ambalo limeacha gumzo kwa wageni wanaoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa – Saba Saba.
Kaparata, baba wa watoto watatu ambaye hakuwahi kuliona darasa lolote, ameweza kutengeneza gari la ‘kifahari’ alilolipa jina la Kaparata ambalo kwa hakika wengi wamevutiwa nalo na wengine kutamani kulinunua.
“Kwani linauzwa kiasi gani? Hili linafaa sana kwenda nalo shamba,” alisema mwananchi mmoja. Mwingine akasema: “Hili ni zuri kama gari aina ya Jeep, la kutokea na familia kwenda kupunga upepo.”
Naam. Walikuwa ni wananchi waliotembelea Banda la SIDO ambako ndiko alikoliegesha gari hilo kwa maonyesho pamoja na bidhaa zake nyingine, kwa kuwa yeye ni miongoni mwa vijana wanaonufaika na fursa za Shirika hilo la Viwanda Vidogo ambalo linawakusanya wajasiriamali na wabunifu pamoja ili kuonyesha kazi zao.
Yeye anafanyia shughuli zake katika eneo la SIDO Vingunguti na hata gari hilo ndiko lilikotengenezewa.
Kaparata 6
“Sikubahatika kusoma hata darasa moja kutokana na matatizo ya kifamilia, huu ni utundu wangu ambao nimekuwa nao tangu nikiwa mdogo. Nilianza kutengeneza magari ya kuchezea kwa kutumia mabati, lakini daima ndoto zangu zilikuwa kutengeneza gari langu mwenyewe, nashukuru Mungu ndoto hizo zimetimia,” anasema Jacob ambaye alizaliwa Mpanda mkoani Katavi kabla ya kuhamia Kigoma ambako baba yake Mzee Louis Jacob alikuwa dereva katika Mamlaka ya Pamba.
Akiwa mtoto wa saba kati ya watoto nane, Jacob anasema kwamba ni wawili tu kati yao waliowahi kuingia katika vyumba vya madarasa ambao ni dada yake wa pili kuzaliwa ambaye aliishia darasa la nne na kaka yake wa tatu kuzaliwa aliyemaliza darasa la saba.
Anasema, baada ya wazazi wao kutengana mwaka 1993, mama yao aliamua kuwachukua yeye na ndugu zake na kurudi Mpanda ambako maisha yaliendelea kuwa magumu mno.
“Elimu ya zamani, hasa ya darasa la sababu, haikuweza kumfikisha popote hata yule kaka yangu, kwa hiyo tulijikita katika shughuli za shamba tu,” anaeleza.
Hata hivyo, anasema kwamba licha ya kutoingia darasani, hivi sasa anajua kusoma baada ya kufundishwa kusoma a, e, i, o, u na mpwawe Sarah William mwaka 1993 na yeye akaziunganisha herufi hizo.

Utengenezaji wa gari
Jacob anaeleza kwamba, gari la ‘Kaparata’ enye muundo tofauti na gari lolote duniani, amelitengeneza kwa kipindi cha miezi mitatu tu kabla ya maonyesho ya mwaka huu ya Saba Saba ambapo limemgharimu kiasi cha Shs. 12,850,000.
“Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtundu sana nikitengeneza magari na vitu mbalimbali kwa kuiga nilivyoviona, ndipo watoto wenzangu wakanipachika jina la ‘Kaparata’, ambalo nimezowea na kuamua kuiita kampuni yangu kwa jina hilo.
“Tangu mdogo nilipenda kuangalia filamu na nilivutiwa na gari moja nililoliona kwenye filamu ya Delta Force ya Chuck Norris (The Flyer 72 Advanced Light Strike Vehicle) nikaapa kwamba lazima nije nitengeneze gari la aina hiyo,” anasema Kaparata.
Kaparata anasema kwamba, gari lake hilo limetumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchini.
“Chassis nimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi limelisuka kwa kutumia brake pipes zinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayo yanatumika kutengenezea mageti,” anafafanua.
Anaongeza: “Nilipomaliza kutengeneza chassis nikaenda kununua injini, diff, gear box na matairi, ambavyo vyote ni vya gari aina ya Suzuki Carry. Unajua Suzuki Carry ni fupi ina futi 10, lakini nilichokifanya ni kuongeza chassis hadi fupi 12. Injini ile ina nguvu sana ila kigari kile kimenyimwa bodi. Sasa gari yangu hii imeonekana kuwa na nguvu, ina kasi.”
Hata hivyo, anasema kwamba, alitumia muda wa wiki mbili kutengeneza chassis ambayo alihakikisha inanyooka na kukaa sawa kabla ya kuendelea na utundu mwingine.
“Hivi sasa nikitembea na gari yangu, hata kama tumeongozana na magari mengine ya kifahari, watu wataitazama gari yangu mitaani na wamevutiwa nayo huku wengine wakinitaka nitengeneze mengine niyauze,” anasema.
Anasema wakati anaanza kuitengeneza gari hiyo vifaa pekee alivyokuwa navyo ni drill machine, grander na welding machine – vifaa vitatu tu, ambapo mabati na vifaa vingine alivinunua.
Kwa kuwa yeye si fundi mchundo, mabati na vifaa vingine aliyapeleka kwa mafundi mchundo ambao walimkunjia kwa muundo na vipimo alivyovitaka yeye.
“Lakini nimeingia hasara kubwa kwa sababu wakati mwingine unampelekea mtu akukunjie bomba au bati, lakini anakosea, inabidi kulitupa na kutafuta jingine.
“Nilipokuwa nayabeba mabati kupeleka kwenye viwanda kwa ajili ya kukunja wengi waliniona kama mwendawazimu, wengine wakanikatisha tamaa na kusema magari wanatengeneza Wazungu miye Mswahili maskini wapi na wapi!” anasema.
Hata hivyo, anamshukuru mkewe Elizabeth William aliyemzalia watoto Beatrice (14), William (10) na Neema (2) ambaye alikuwa akimtia moyo kila wakati aendelee na ubunifu wake.
“Unajua hata kule kwenye viwanda nilikokuwa napeleka hawakuamini, kwa sababu nilipoyabeba mabati wengine walidhani nakwenda kutengeneza ndoo, lakini baada ya mabati hayo kukunjwa kama nilivyotaka, wote walishangaa,” anasema.
Ukilitazama gari hilo kwa mbali unaweza kudhani ni aina mpya ya Jeep ingawa muundo ni tofauti kabisa, na kama utalikaribia utashangaa kuona vikorombwezo vingi.
“Hiki kioo cha mbele ni cha Land Cruiser ila nimekata mashavu ya pembeni. Indicator ni za Bajaj aina ya TVS, shoo ni za vifaa mbalimbali vya magari. Nimeweka vent kama za Ranger za kuingizia hewa kwenye air cleaner na mengine kibao,” anasema.
Kaparata anasema kwamba, ubunifu ni gharama kubwa, lakini mahali alipofikia kwa sasa anajiona kama ni mhandisi aliyebobea ingawa kikwazo ni mtaji pamoja na kutambulika na mamlaka zinazohusika.
“Mheshimiwa Rais Magufuli amesema anataka kuona Tanzania yenye viwanda ambayo ndiyo nia pekee ya kutengeneza aira kwa sisi vijana, sasa mimi nimeamua kuanza bila kupata msaada wa mtu yeyote mpaka nimekamilisha, ninachokihitaji kwa sasa kwanza ni kutambuliwa na serikali kwa ubunifu wangu, halafu niweze kupatiwa mtaji na mazingira bora zaidi ya kufanyia kazi.
“Kama leo nitaamua kutengeneza gari nyingine kama hii, ninaamini ndani ya mwezi mmoja nitakuwa nimeitengeneza na itakuwa bora kuliko hii kwa sababu nimejifunza makossa yote wakati nahangaika na hii hapa,” anaongeza.

Amewezaje kumudu gharama?
Kaparata anasema kwamba, mpaka anakamilisha kutengeneza gari lake hakuchukua hata senti tano ya mtu bali ni fedha zake mwenyewe kutoka katika vyanzo vingine.
Anasema kwamba, wengi walimcheka na kusema kama anazo fedha za kuchezea bora akawape maskini kwa vile asingeweza kufanikiwa kutengeneza gari, lakini kwa kuwa alikuwa na ndoto zake akaamua kuyapuuza maneno yao na kukwangua kila akiba aliyokuwa nayo kutimiza hayo malengo.
“Mimi ninafanyia kazi zangu pale SIDO Vingunguti, zaidi natengeneza mashine za kutotolesha vifaranga ambazo kidogo kidogo ndizo zinazoniingizia fedha, hivyo hata fedha za kutengenezea gari hili zimetokana na kazi hizo,” anasema.
Anaongeza kwamba, licha ya kutokusoma, lakini utundu na ubunifu wake vinamwezesha kuendesha maisha yake na amekuwa tegemeo kubwa kwa ndugu zake wote.
Amewaasa vijana wengine waliosoma na hawana ajira pamoja na wale ambao hawakubahatika kupata elimu kutokukata tamaa, bali wanaweza kutumia vipaji na nguvu walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu kufanya maendeleo.

Tuesday, 5 July 2016

Why Failure Is the Key to Success for Women

When I bodysurfed with my three brothers as a kid, I didn’t hate wiping out as much as I hated my brothers’ laughing at me when I emerged from the wash of a big wave spluttering and gasping for air, swimsuit askew. I had a choice, I could either stop bodysurfing (and thus get left behind) or get used to getting dumped. Eventually I figured out a solution: wipe yourself out so you get used to it and don’t dread it as much.

What I discovered after a few self-imposed poundings was that if you can find the sand, you can find the air; it’s in the exact opposite direction. And the wave is always happy to introduce you to the sand. Usually it was right where my face was planted. So, if you let the surf fling you about a bit, you can eventually get the sand under your feet and emerge from the water with your swimsuit and composure more or less intact. I still got dumped, but I did it with a little more dignity.
What I now realize I was learning to do, was fail.
Women need to fail. They need to fail hard and they need to fail often. It’s the only way they’re going to succeed. It seems cruel to say that. For many women, lack of success is as familiar as breakfast cereal, except they eat it three meals a day. But a new poll conducted for Time and Real Simple magazines suggests that an unwillingness to fail or a fear of doing anything that could lead to a washout might be one of the pinch-points that is impeding women’s progress to the head office. Failures happen to everyone, but these poll results suggest that women fear them more and perhaps don’t bounce out of the surf from them quite so readily.
As part of an ongoing national conversation about why women occupy leadership roles in much smaller numbers than their education, their ability and just simple math would suggest, the polling company Penn Shoen Berland asked 1000 women about success, what it meant to them and what they felt it took to be successful. They also asked 300 men some of the questions to offer a point of comparison. The women ranged in age from 20 to 69 and about 40% of them were in paid employment.
Some of the poll data confirmed what our gut tells us: for women success is less like a spearfishing trip and more like collecting shells on the beach. It’s not a linear process, with just one goal in mind. Secondly, motherhood has a huge influence on women’s outlook, both in her definition of success (it widens) and in her bandwidth (it bifurcates). Other results were more surprising: being good at their jobs was vastly more important to women than men in our survey. And almost half of them believe they are paid less than men for doing an equivalent job.
The biggest bogeyman in the discussions about what’s holding women back is a lack of confidence. Why do women not ask for higher salaries when negotiating? Confidence. Why are women the last to put up their hands for a promotion? Confidence. Why don’t more women run for office? Confidence. Plus all the guff they’d have to take about their hair.
That idea may need refining. One of the clearest finding to emerge from the Time/Real Simple poll is that women aren’t much less confident than men. About 45% of people regardless of gender regard themselves as confident. But many more women—nearly 80%—say it’s an important part of success. Only 63% of men do. That is, women and men are confident in equal measure. But more women think it’s important.
Female workers, the poll numbers show, labor just as hard, believe they are just as qualified, and have as much professional respect as their peers. That sounds a lot like confidence. Yet they just don’t seem to swim for the waves the men do. Roughly three quarters of both men and women said they would not want their boss’s job. But, if offered the position, more than half the men would take it anyway and fewer than a third of the women would. Why do the men believe they could do the job and the women don’t?
The demands of motherhood may be one of the forces at play here, but it’s not the only one. According to the poll, women’s hunger for success dwindles as they age. Almost 75% of women in their 20s regard it as very important to be successful. By their 40s and 50s—the age at which people often become senior executives—only 50% of the women feel the same way. About half the 20 year old women surveyed considered it vital to get promoted. Less than a third of women in their 40s felt the same way.
If this were all just because women wanted time and energy and bandwidth for that resource-intensive home-based start-up called parenting, then it follows that their desire to contribute to the success of their team or to work as hard would ebb too. But it doesn’t wane at all, no matter the age. Women seem to want to put in the time and effort, but not to expect the rewards. Or the status.
Perhaps there’s an answer in women’s attitude to innovation. More than 40% of women believe the ability to innovate is one of the passports to success. But only a few women think they carry that passport. What do confidence and innovation have in common? They can’t be learned without making mistakes. Acquiring them without going through failure is not an option. Failure often hurts, but as Lawrence of Arabia said (in the movie, at least) “the trick is not minding that it hurts” and swimming back through the swell to try again. Women seem less eager to do this. What is innovation, after all, but failing to solve a problem a little less badly each time?
One nugget from the poll encapsulates this quite neatly: to prepare for a big presentation women are more likely than men to do a lot of research and give themselves a pep talk. Men, on the other hand, were more likely than women to give themselves a treat, take meds or practice their power pose in the bathroom. The men are much more likely to revel in the high wire act, to enjoy the risk, than women. (Either that or their meds are amazing.)
It makes sense that women are risk averse. That tendency has protected them and their offspring for centuries. It fortified those pioneering female business leaders who were under a higher level of scrutiny even as recently as this decade. But if women hope to get to the corner office, to that mythical realm that smells like Y chromosomes and golf shoes, they have to be prepared to fall on their faces. And get back on up again.
So here’s a suggestion. Go forth, ladies and louse up. Muff it. Make a blunder. Botch it up royally. Make a complete balls of it. The guys do it all the time. Just before they get promoted.