Tunapozungumzia suala la mtoto .tunamlenga baba na mama.
Inanisikitisha sana kuona baba anaoa mama ambae anamtoto wa baba mwingine.wanawaita watoto wa kambo.
Yule baba anamuahidi mama "nitakutunza pamoja na mwanao".
Baada ya muda fulani wa miaka kadhaa wanapata watoto .Hapo baba anaanza visa kwa yule mtoto amesahau ahadi zake kwa yule mama.
Kibaya zaidi sana ukute yule mama aliolewa hana kazi; sasa baada ya muda yule
baba anaanza kumnyanyasa yule mtoto tena kwa ukatili mbaya na mama
anapoingilia anapigwa pamoja na mwanae .
Hapo ndo nashindwa kuwaelewa kama
hawajui kwani watoto ni Taifa la kesho.na
mtoto wa mwenzio ni wako .
Akina Baba badilikeni,suala la kunyanyasa watoto kwa kigezo sio wa kwako ni kosa
kubwa. Kumbuka mtoto wa mwenzako ni mwenzako.
Veronica Sheiza- Muuguzi na mtaalam wa
masuala ya mahusiano na saikolojia