Tuesday 8 March 2016

NINA SABABU YA KUMSIFIA MAMA YANGU KWA NIABA YA WANAWAKE WOOTE DUNIANI JUU YANGU -2 !!

INAENDELEA>>
Basi siku moja nikiwa shuleni mwaka 2000 Nilikaa na kuwaza "nawezaje kwenda kwa baba akanisomeshe" ikanibidi nibuni barua as if baba ameniandikia so nikaaandika barua kisha nikarudi nayo hadi nyumbani kwa Babu na kumwambia kuwa kuna barua imetoka kwa baba Dodoma ameniita tukajadili mambo ya masomo. Basi babu bila hiyana ilibidi aniruhusu niende akanipa ramani hadi ya dodoma kwa sababu dodomaa sikuwahi kufika nikiwa mkubwa tangu nilipopelekwa nikiwa sijielewi wakati naumwa typoihd na malaria.
Nakumbuka nauli ilikuwa 3000 nami nilikuwa na 5000 nikapata "piga bao au land rover " hadi dodoma na nikafika kwa baba naye akashangaa nimefikaje na nini kimenipeleka.
nilipofika nikajieleza kuwa nahitaji kusoma dodoma ndio ikawa tumekubaliana mwezi ujayo niende kujadili zaidi .
Nilirudi manyoni kwa furaha nikamkuta Babu na kumjuza ya Dodoma . Ila sikumwambia kama ninataka kuhamia dodoma kwa sababu nilijua kabisa asingefurahi wala mama asingekubali kwa sababu mama alishaamua kunisomesha hadi pale atakapoona nimefikia napohitaji.
Mwisho wa mwezi nikarud dodoma ndio nikazamia bila hata kuaga mtu kuwa sirudi Manyoni. Babu akasubiri kama kawaida yake eric jumatatu atakuja hakuona mtu jumanne hakuona wiki mwezi ikabidi atume ujumbe Jose aka eric tangu ameenda dodoma hajarudi .
Mama alishtuka sana ikabidi aje hadi Dodoma Mpunguzi na kunikuta kwa baba namwagilia bustani ya nyanya, alihuzunika sana akaniuliza umeamua kuacha shule Jose?? nikamwambia "mama nimekuja baba anisomeshe" mama alinitazama akasema "sawa ila ukiona pagumu rudi manyoni usome" UPENDO WA MAMA UNAZIDI KUBUBUJIKA JUU YANGU .
Basi akageuza na kurudi kazini kwake na kumjuza Babu kuwa mimi Jose au Eric nitasoma secondary next year 2001.
CHANGAMOTO ZA ELIMU.
Nilianza kusoma vizuri mama akiwa ananifuatilia na Baba akinisomesha pale Merriwa sekondari.
Hali ilianza kubadilika kimahusiano baina yangu na Baba nikawa nasoma kwa shida kisaikolojia kiasi kwamba nikaanzakuon ndoto zangu zinadidimia kabisa.
Wakati nikiwa kidato cha tano (NAKUMBUKA) ulitokea mzozo mkubwa sana kati yangu na Baba ,hadi akanifukuza na niliapa MIMI NA SHULE BASI,KUANZIA LEO SITAKI KUSOMA.
Nilirudi kwa baiskeli kutoka dodoma hadi kijijini manyoni kwa mama na kumsimulia mkasa mzima huku machozi yakinitoka. Niliumia sana lakini sikuwa na maamuzi zaidi ya kuacha shule tu niwe mtu mwingine kabisa.
Baada ya kumwambia nakumbuka mama alikuwa kakaa mezani kaangalia mashariki mahali dodoma ilipo huku machozi yakimtoka akanambia JOSE KESHO UNARUDI SHULE UTAKAA POPOTE NITAUZA KILA KITU KUHAKIKISHA UNASOMA niliumia sana kuona mama yangu anatoa machozi ili mimi nisome. Kweli Kesho yake ikawa hivyo akanipa hela mama nikageuza dodoma ndio nikaenda kumalizia elimu yangu ya kidato cha sita .
Baadae nikaenda chuo na ndio huyu eric samuel mfamuyo.
IKO HIVI
1. Bila usimamizi wa mamaa familia yetu ingeshasambaratika siku nyingi
2. Bila mama tusingefikia ndoto zetu kwa asilimia kubwa ktoka kwenye msingi
3.BiLa mama mimi na wadogo zangu tusingekuwa kama tulivyo.
4. Bila mama huenda nisingeishi kabisaaaa maana nilishaamua maamuzi magumu
.Bila mama nisingemjua Mungu huyu ninayemuabudu na kumtukuza.
NDIO MAANA NASEMA MAMA KWANGU SIKUMPA SIFA ZA KISIASA NIMEJIKUTA NAKUMBUKA MEEENGI SANA KWA SABABU YEYE NDIYO BASEMENT YA MAFANIKIO MAKUU TULIYOYAPATA HUKU TULIPO NA BABA KWA SEHEMU YAKE.
NINAUJUA MCHANGO WAKO KWANGU DAIMA MAMA YANGU NA SITOKUANGUSHA MAANA HATA NIKIKUAHIDI MENGI KIASI GANI SIWEZI KUFIKIA KIWANGO CHA UPENDO WAKO KWANGU.
MUNGU AZIDI KUKUBARIKI MAMA YETU KIPENZI DAIMA.
www.smgeorg.blogspot.com

· NINA SABABU YA KUMSIFIA MAMA YANGU KWA NIABA YA WANAWAKE WOOTE DUNIANI JUU YANGU-1 !!!

Eric Samuel thinking about my mother "mamabetty".
A. KABLA YA KUZALIWA MIMI Eric Samuel
Mama aliwahi kunambia kuwa kati ya watoto walomsumbua sana kipindi cha ujauzito basi mimi Nilivunja rekodi,nilimtesa sana ,sasa sijui kwa sababu ndio mtoto wa kwanza wa kiume lakini all in all Mamabetty alisumbuka sana wakati amenibeba tumbo.
B. BAADA YA KUZALIWA(WAKATI NI MTOTO MDOGO CHINI YA MIAKA MITANO)
1. Alinambia nililiwahi kuumwa sana typhoid na malaria wakati ninakama miaka mitano huko kijijini Ikasi Manyoni-Singida ambapo tulikuwa tunaishi huko walipokuwa wanafanya kazi kiasi kwamba sikuongea kwa muda wa wiki mbili nimelala tu ikabidi wanipeleke Dodoma hospitali ya mkoa nikiwa kwenye hali mbaya wodi namba 13 ya watoto. Kufika pale nikawekewa drip za maji kama chumba zaidi ya tatu hali ilikuwa mabaya .
Baada ya muda nikawa nafumbua macho nikawa at least nafumba na kufumbua hali ile iliwapa mashakaka wauguzi ikabidi wamwambie mama chukua dawa hizi utaendelea kumuuguza home. Mama akanibeba na kurudi tena huko kijijini kwenye kituo cha kazi, ambapo usafiri pia ilikuwa shida . Basi akiwa njiani basi lilipoishia akiwa anatembea kwa miguu mimi nikiwa mgongoni siongei wala kulia wala kufanya chochote tangu nitoke hospitali nilipokuwa nimelazwa, jua lilikuwa kali akaona apumzike chini ya mbuyu akawa amenilaza chini nikazinduka nikamuita na kumwambia "mamaa maji,mama maji" hapo nikampa mama matumaini nikapoa kuanzia pale nilipokunywa maji. MAMA NI ZAIDI YA MAMA.
2. Wakati nimtoto wa kubebwa mgongoni siku moja alipokuwa anatoka Saranda anaelekea Londoni kwa miguu huko wilaya ya manyoni aliwahi kupotea njia jioni hivyo alizunguka akiwa amenibeba mimi mgongoni na begi kichwani Mama betty alizunguka kutafuta njia msituni ambao ulikuwa na wanyama wakali kama chui tembo na simba lakini juhudi hizo hazikufanikiwa. Kuona imefika usiku sana saa tatu amekosa la kufanya ikabidi aingie kwa kujipenyeza kwenye usio wa miiba kuingia kwenye shamba la mtu ,akatoa nguo kwenye begi na kutandika chini ,Mama yangu akaomba sala pale akanilaza chini tukalala hadi asubuhi. Mungu alivyomwema sikulia wala kumsumbua wala kudhurika na kitu chochote hadi asubuhi. Ndipo alipotafuta njia na kuipata hadi akafka kijijini na kwaacha watu midomo wazi kuwa amewezaje kupata ujasiri wa kulala msituni na mtoto mdogo sehemu ambayo ni hatari bila kudhurika.
BAADA YA KUKUA KWETU NA FAMILIA YETU.
A. Aslimia kubwa sisi maisha yetu ya utoto tumekulia kwa mama.Pale baba alipohamia Dodoma kikazi watoto watano tulikuwa chini ya uangalizi wa mama. Nikiwa darasa la tatu Baba alihamia Dodoma hivyo sisi tulibaki kwa mama ,na mama alitusimamia mimi na wadogo zangu na dada yetu Hilder mpaka tukamaliza shule ya msingi kwa kipato cha kawaida tunasoma kwa hela za kuuza vitumbua na huku tukilima mazao kama mahidi pamba,alizeti,ufuta namaharagwe hivyo ndivyo vilikuwa vyanzo vyetu vya mapato chini ya usimamizi wa mama.
Ili kuhakikisha mwanae nasoma vizuri Mama alinihamishia mjini ambapo nilimalizia shule ya msingi manyoni pale manyoni mjini ndipo nikajiunga na mwanzi sekondary mwaka 2000 nikiwa naishi kwa Babu mzaa Mama Marehemu Mzee Joseph Kwana .
INAENDELEAAA>>>>>>