Ni upi umiliki wa ardhi, nyumba na kampuni?
Umiliki wa mali yoyote inayo hamishika au isiyo hamishika unaelezewa katika haki za kumiliki. Haki za kumiliki ni pamoja na haki za kumiliki mali, kujipatia ( kupitia kununua, zawadi au mirathi), kusimamia, kufuruhia na kuuza mali zinazoshikika na zisizoshikika pamoja na ardhi, nyumba, pesa, akaunti ya benki na mali nyingine kama mifugo na mazao.
Kwa nini haki za wanawake kumiliki mali ni muhimu?
Kwa nchi kuendelea ni muhimu kwa wanawake kupewa haki za kumiliki. Haki za kumiliki mali kwa wanawake zinaboresha usawa wa kijinsia ambao unapelekea maendeleo. Ukosefu wa haki hizi hupelekea kutokuendelea kwa wanawake na kuzidi kuwadidimiza. Kutokana na Shirika la Kimataifa la makazi, kwa kila nchi 1 katika 4 zinazoendelea kuna sheria zinazo wakandamiza wanawake kumiliki mali. Kama ilivyoelezwa na Benki ya Dunia, nchi zenye sheria zisizo na usawa katika mirathi pia hazina haki na usawa katika kumiliki mali.
Hivyo haki ya kumiliki mali kwa wanawake ni muhimu kwani ndiyo inayompa mwanamke ulinzi wa kiuchumi, hadhi ya kijamii na kisheria na hivyo kuweza kudumu. Umiliki wa mali na ardhi unawawezesha wanawake na kuwasaidia kupata kipato na ulinzi wa kiuchumi. Bila ya haki za kumiliki, wanawake wanakosa usemi katika maamuzi ya nyumbani, na wanakosa haki zao katika kipindi cha matatizo kama vile talaka au kifo cha mume au hali yoyote yenye utata. Ukosefu wa haki za kumiliki pia unapelekea migogoro ya kifamilia na kijamii.
Ni zipi haki za wanawake kumiliki mali?
Chini ya sheria za kimataifa, wanawake kama ilivyo kwa wanume, wana haki sawa za kumiliki mali. Haki hizi ni kwa mali zinazohamishika na zisizohamishika ( au zinazoshikika na zisizoshikika). Ijapokua katika nchi nyingi za dunia, haki za kumiliki mali kwa wanawake zinazuiwa na mila, desturi, dini, tamaduni, tabia za kijamii na sheria.
Ni masuala gani yanahusishwa na haki za wanawake kumiliki mali?
Kama yalivyo masuala mengine ya haki za binadamu, haki za wanawake kumiliki mali zinahusishwa na matendo ya unyanyapaaji katika mirathi, kilimo, uongozaji wa kijinsia katika rasilimali za kiuchumi, haki ya kufanya kazi na migogoro ya kifamilia au unyanyasaji wa wanawake.
Kuwapatia wananawake haki sawa za kumiliki mali kuna maanisha kupunguza vitisho vya unyanyapaaji, migogoro ya kifamilia na kijamii na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu. Pia ina mchango chanya katika kuhusisha wanawake katika siasa na kuwawezesha wanawake kwa ujumla.
Ni zipi kanuni za kimataifa juu ya wanawake kumiliki mali?
Sheria za kimataifa za haki za binadamu zinashurutisha ulinzi sawa katika haki ya kumiliki mali kwa wanaume na wanawake. Haki za kumiliki ni haki za binadamu. Haki za wanawake kumiliki mali ikiwa ni pamoja na ardhi ni haki za binadamu zisizowezwa kukiukwa na pia zinahusishwa na kiwango cha maisha chenye kujitosheleza, haki ya kupata makazi na uhuru wa kutokufukuzwa katika makazi. Haki hizi zinasimamiwa na vyombo vifuatavyo vya kimataifa.
International Instruments/Convention
| Relevant Article | Article Text |
Azimio la pamoja juu ya haki za binadamu | 17 |
Kila mtu ana haki ya kumiliki mali mwenyewe ama kwa pamoja na wengine.
Si sawa kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake
|
Maazimio ya kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake | 13-16 | Serikali kuhakikisha kua wanawake na wanaume wanapata haki sawa katika mafao ya familia, kupitia upya masuala ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuhamisha makazi, wanafurahia kiwango cha maisha chenye kujitosheleza hususani yenye kuendana na makazi, kua na haki sawa katika kusaini mikataba na kusimamia mali, kua na haki sawa kwa wanandoa katika kumiliki, kujipatia/kutafuta, kusimamia, kufurahia na kuuza au kugawa mali bure ama kwa kuzingatia thamani fulani |
Maazimio yote ya kimataifa juu ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na yale ya haki za kiraia na kisiasa yanashurutisha kutokuepo kwa ubaguzi wowote katika misingi ya kumiliki mali. |
Jukwaa la makubaliano kwa vitendo la Beijing ( lililotangazwa mwaka 1995) limeshurutisha kwamba haki za wanawake kurithi na kumiliki ardhi na mali zitambulike na serikali iweke sheria na kupitia mikakati mipya ili kuondoa utofauti. Haki za wanawake kumiliki mali pia zimeongelewa katika Malengo ya maendeleo ya Milenia, hasahasa goli la 11 linalozungumzia kuondoa umasikini uliokithiri na goli la 3 linalozungumzia usawa wa kijinsia. Kufikia malengo haya kunategemeana sana na uzingatiaji wa haki za wanawake kumiliki mali.
Ni vitu gani vinapelekea kuvunjika kwa haki za wanawake kumiliki mali?
Sababu kuu hasa zinazopeleka haya ni kuwapo na sheria za kibaguzi, mila na desturi mbovu, mtizamo hasi juu ya haki ya wanawake kumiliki mali, utofauti wa mamlaka na mfumo mbovu wa mahakama. Wanawake wanaopigania haki zao huitwa wenye tamaa.
Ni yepi matokeo ya ukiukwaji wa haki za wanawake kumiliki mali?
Ukiukwaji wa haki hizi hupelekea wanawake kua wategemezi kwa wanaume. Wanawake hubakia masikini na hukosa fursa sawa na wanaume. Hali hii huwafanya waishi maisha duni na kila mara katika hatari ya kunyanyaswa na wazazi na mashemeji. Matokeo ya vitendo hivi ni nchi kushindwa kuendelea.
Ni zipi faida za haki za wanawake kumiliki mali?
Haki za kumiliki zinajumuisha faida nyingi kwa wanawake na familia zao kwa kuongeza uwezo wao wa kujadiliana juu ya bei au malipo,ulinzi wa kijamii na kujitawala kiuchumi. Haki za wanawake kumiliki mali zinaongeza uwezo wao katika majadiliano ndani na nje ya nyumba na kuonekana viongozi.
Katika nchi zinazoendelea wazazi hutegemea watoto wao. Watoto huwajali wazazi wao kama wazazi wataendelea kua na nguvu na mali zao zinazozalisha na wanafurahia haki za kumiliki. Haki za kumiliki huwapa wanawake uwezo wa kiuchumi ikiwa wanaishi na wazazi wao au waume zao. Kama watakosa haki hizi, wanawake watabaki wategemezi na kazi zao za nyumbani na kazi nyingine hazitoonekana na wala kusahauliwa.
Maazimio yote ya kimataifa juu ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na yale ya haki za kiraia na kisiasa yanashurutisha kutokuepo kwa ubaguzi wowote katika misingi ya kumiliki mali kwa mtu.