Tuesday, 10 May 2016

HEBU TUKOMESHE MIMBA ZA UTOTONI KWA WATOTO WALIOPO SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI TANZANIA

Mtoto ni rasilimali ya leo kesho na keshokutwa. 
Kitendo cha kuwanyamazia wale wanaowatongoza au kuwarubuni watoto hawa ikiwepo mabinti wa shule za sekondari mijini na vijijini ni kosa kubwa sana tunalolifanya sisi kama wanajamii.
Suala la kuwakemea hawa wachafuzi wa watoto wetu wanaosoma nijukumu la kila mtoto,kijana,mtu wa makamo na  mzee   yeyote yule kuwalinda watoto hawa wasiharibiwe malengo yao na watu wachache wenye mihemuko ya uharibifu.
Maisha mazuri ya watoto wanaosoma hasa wa kike yanategemeana na jinsi ambavyo sisi kama jamii tunawalinda na kuwaheshimu kama watu muhimu kwa jamii yetu.
Hawa ndio wabunge,makatibu marais, mawaziri na wakurugenzi wa kesho lakini ndio maafisa mipango wa kuanzia usiku wa leo na kuendelea.
Tuwathamini watoto wa kike, tuache kuwarubuni , tuwasaidie kutimiza ndoto zao.
kampeni hii imeletwa kwenu na Shirika lisilo la kiserikali na Masuala ya Jinsia.
Social Mainstreaming for Gender Equality Organization
P.O.BOX 6444
Morogoro, Tanzania
Barua pepe: smgeo2015@gmail.com


No comments:

Post a Comment