Tuesday, 10 May 2016

NYIE WABABA "MSIWANYANYASE WATOTO WA KAMBO" TIMIZENI AHADI ZENU KAMA MLIVYOWAAHIDI MAMA ZAO KABLA YA KUWAOA KUWA MTAWATUNZA!!

na Veronica Sheiza,
Tunapozungumzia suala la mtoto .tunamlenga baba na mama.

Inanisikitisha sana kuona baba anaoa mama ambae anamtoto wa baba mwingine.wanawaita watoto wa kambo.

Yule baba anamuahidi mama "nitakutunza pamoja na mwanao".


Baada ya muda fulani wa miaka kadhaa wanapata watoto .Hapo baba anaanza visa kwa yule mtoto amesahau ahadi zake kwa yule mama.

Kibaya zaidi sana ukute yule mama aliolewa hana kazi; sasa baada ya muda yule 

baba  anaanza kumnyanyasa yule mtoto tena kwa ukatili mbaya na mama 

anapoingilia  anapigwa pamoja na mwanae .

Hapo ndo nashindwa kuwaelewa kama 

hawajui kwani watoto ni  Taifa la kesho.na 

mtoto wa mwenzio ni wako .

Akina Baba badilikeni,suala la kunyanyasa  watoto kwa kigezo sio wa kwako ni kosa 

kubwa. Kumbuka mtoto wa mwenzako ni  mwenzako.

Veronica Sheiza- Muuguzi na mtaalam wa 

masuala ya mahusiano na saikolojia