Wednesday, 2 March 2016

WASTANI WA WAZEE 500 HUUAWA KILA MWAKA KUTOKANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA MIKOA YA KANDA YA ZIWAMratibu wa Hifadhi ya Jamii Julius Mwengela akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Tatizo la mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Kanda ya Ziwa limeendelea kuwaumiza vichwa wadau mbalimbali wanao jihusisha na masuala ya maendeleo ya jamii hivyo kufanya jitihada kadhaa zinazolenga kutokomeza ukatili huo.

Shirika la MAPERECE lenye makao makuu yake wilayani Magu leo limeketi na waandishi wa habari jijini Mwanza kwa lengo la kuainisha masuala ya wazee ikiwemo changamoto wanazokumbana nazo mwisho wa siku yajulikane kwa mapana zaidi ikiwa ni pamoja na utatuzi wake.  
Wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kikazi zaidi.
Vitendo vya mauaji ya wazee vimezidi kuongezeka na kusambaa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. takwimu kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1998- 2001 kulikuwepo na matukio 17,220 ya kuwadhalilisha wazee namauaji 1,746 kutokana na imani za uchawi.

Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu ya mwaka 2009 ilionyesha kuwa wanawake wazee 2,583 walikuwa wameuawa katika mikoa minane ikiwa ni wastani wa mauaji 517 kila mwaka.

Taarifa kutoka mkoani Shinyanga pia zinatisha kwani wanawake wazee 241waliuawa mkoani humo pekee kati ya januari 2010 na juni 2011.

Wakati mauaji yaliyo mengi yanatokea mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Kagera Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa tatizo la mauaji linasambaa kwenye mikoa mingine ya Tanzania
Siyo sahihi kusema kuwa juhudi zote za serikalina wadau wengine hazina nguvu. Hata ahivyo ni ukweli kuwa jitihada hizi haziratibiwi na serikali na hivyo kukosa ufuatiliaji ambao ungeweza kuleta mahusiano baina ya wadau na kuleta uwajibikaji kwakutoa maamuzi kupambana na mauaji ya wanawake wazee.
Lengo kuu la kusanyiko hili ni kuwapa upeo waandishi wa habari juu ya masuala ya ukatili ufanywao kwa vikongwe nchini ili kutetea haki stahiki za wazee na watoto walio katika mazingira hatarishi wanayoishi pamoja na wazee.
Mapungufu mengine ni pamoja na:
Kukosekana na mipango, fedha na nguvu baina ya Wizara na mashirika yanayohusika na kukabiliana na mauaji ya Wazee.

Mauaji ya wazee kuchukuliwa kwa sura ya imani za uchawi na hivyo kujenga dhana kuwa haiwezekani kuyathibitisha pasipo shaka mahakamani kama ilivyo  kwa kesi nyingine za mauaji.

Mara nyingi viongozi wa serikali, wanasiasa na asasi za kiraia hubaki kimya wakati makosa makubwa dhidi ya binadamu yanapofanyika.

Mipango ya kukabiliana na tatizo hili kukosa uwezeshwaji (Fedha)

Kutotungiwa sheria kwa sera ya Taifa kwa wazee kwa miaka kumi sasa.

MAPENDEKEZO /JINSI YA KUKABILIANA NA TATIZO HILI
Bado tunaamini Serikali ikiwaratibu kikamilifu wadau wote patakuwepo na nia ya dhati na uwajibikaji wa taasisi zote za serikali zinazohusika pamoja na wadau wengine tutaweza kuleta mabadiliko yatakayoondoa kabisa mauajia ya wazee nchini.