NA EXAUD MTEIIkiwa leo ni siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji duniani imeelezwa kuwa bado mapambano dhidi ya ukatili huo hapa nchini kwetu Tanzania yanahitaji nguvu ya ziada kwani bado baadhi ya mikoa imekuwa sugu katika vitendo hivyo ambapo serikali imetakiwa kuchakua hatua mara moja juu ya watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo.
Akizungumza na wanahabari leo mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akiwakilisha mashirika zaidi ya 15 yanayohusika na ukeketaji nchini Tanzania wakili HAROLD SUNGUSIA amesema kuwa mwaka 2014 umeshughudia watoto wengi wakikeketa, pamoja na jitihada za kutokomeza vitendo hivyo ambapo ametolea mfano wilaya ya tarime pekee takribani watoto 1400 walikeketwa na watoto hao ni kutoka katika koo za bukira watoto 212,bukenye watoto 230,iregi watoto 800,pamoja na nyabasi watoto 160,ambapo ni idadi kubwa sana na ikizingatiwa kuwa ni wilaya moja tu.
Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria zinazolikemea tatizo hilo bado cha kusikitisha ni kuwa mila hii imekuwa ikitekelezwa kwa kasi sana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania katika baadhi ya jamii zetu.
“tunaitaka serikali kwa kupitia jeshi la polisi kusimamia sheria na kuwachuklia hatua za kisheria watu wote watakaobainika kufanya vitendo hivi”amesema SUNGUSIAAmeongea kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, na kosa la jinai huwa haliishii yani halina ukomo wa muda hivyo wanatarajia kuwa kama serikali inamaanisha kweli kupinga ukeketaji huo basi iweze kufwatilia huko vijijini na kuwabaini wale wote wanaoshiriki kukeketa watoto na kuwachukulia hatua stahiki
Baadhi ya mashirika ambayo leo wameungana kwa pamoja kupinga vitendo hivyo ni TAWLA,TAMWA,DIAC,CCT,WORDVISSION,NAFGEM,AFNET,WOWAP,CDF,WLAC,TGNP MTANDAO,WILDAF,BAKWATA,TGNP pamoja na HOUSE OF PEACE
No comments:
Post a Comment