Wednesday 2 March 2016

MABADILIKO HUANZA TARATIBU SANJARI NA MAFANIKIO !!


Ni kweli huwezi kubadilika leo, lakini unaweza kufanya kitu leo kitakacho ibadili kesho yako. Haijalishi ulizaliwaje, hiyo ilikuwa ndiyo ya leo. Haijalishi ni nini kilitokea miaka mitano nyuma, miaka kumi iliyopita...huwezi kubadili miaka hiyo maana tayari ilishapita. Lakini unachoweza kufanya leo ni kijipanga upya tena, unaweza kufanya maamuzi mapya leo; maamuzi ambayo yataibadili kesho yako.
Kataa kuwa zezeta katika maendeleo, kataa maisha yako kuwekwa pembeni. Leo wacha nikujulishe kitu ninachokiamini katika kesho yako. Nina sababu ambayo inanifanya niamini katika kesho yako. Ninaamini kwamba kama ukiamini maneno haya na kuyafanyia kazi, lazima utapata mabadiliko katika maisha yako.
Hakuna mtu aliyeumbwa ili awe masikini; ndiyo unaweza ukawa umezaliwa katika familia masikini lakini ukweli ni kwamba hujazaliwa ili uwe masikini. Ndiyo unaweza ukawa umewekwa katka nchi masikini lakini ukweli ni kwamba hukuwekwa katika nchi hiyo ili uwe masikini.

Natamani uelewe hii maana ya neno "Utu uzima" utu uzima ni kuwajibika. Pindi unapokuwa mtu mzima huwezi kukwepa majukumu kwa maisha yako. Kubali kuwa muajibikaji katika uwezo ulio nao. Kuna wengi leo wanalilia msaada na kwa sababu hakuna majibu katika wito wao wa msaada hujisiki maumivu makali ya kupuuzwa katia mioyo yao. Hapana, usikubali kukata tamaa. Amini katika kile ambacho MUNGU Alikiumba. MUNGU Alikuumba wewe na wala MUNGU Hakukuumba uwe mtu wa kushindwa. Amini kwamba MUNGU Ana kusudi fulani maishani mwako. Kuna nafasi yako na wewe ya kuwa mtu aliyefanikiwa hapa duniani.

Kuna vitu vichache vya kuzingatia ili kufika mafanikio yako. Mojawapo ya mambo hayo ni muda. Tumia muda vizuri. Tumia muda wako katika kuleta maendeleo makubwa. Kama wewe ni mwimbaji...fanya uimbaji wako uwe wa kuigwa na wala si wa kuiga. Kumbuka huwa hakuna muda wa ziada hivyo tumia muda wako vizuri. Mafanikio humsubiri mtu anayeyatafuta. Mafanikio yapo kwa mtu asemaye "nitaamka mapema niende kazini" na huamka. Mafanikio yapo kwa mwanatunzi asemaye "Nitajisomea vitabu vya kutosha ili nifaulu".
Kwa hiyo usipoteze muda wako mwingi kuangalia runinga ama televisheni....usipoteze mda wako ukiangalia video za tamthiliya masaa 24. Panga kutazamwa mwenyewe kwenye runinga siku moja na wala usikubali kutazama wengine.
Utakuta mtu anasifia kazi nzuri zilizofanywa na wengine.....jipange nawe siku moja watu wasifie kazi nzuri uliyoifanya.

No comments:

Post a Comment