Tuesday 1 March 2016

Ukeketaji ni tatizo la kimataifa, utokomweze ifikapo 2030:UNFPA/UNICEF


Kusikiliza / Hamishia
Asmah Mohamed, mtoto wa miaka 6, akifarijiwa na mama yake baada ya kukeketwa, nchini Kenya. Picha ya UNICEF/NYHQ2005-2229/Getachew

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji , shirika la idadi ya watu duniani UNFPA na la kuhudumia watoto UNICEF yamesema ukeketaji ni tatizo la kimataifa lililokwenda mbali zaidi ya Afrika na Mashariki ya Kati ambako vitendo hivyo vimemea mizizi. Sasa umeathiri jamii za Australia, Asia, Ulaya na Amerika ya Kusini na Kaskazini.
Kwa mujibu wa mashirika hayo idadi ya wasichana na wanawake walio katika hatari itaendelea kuongezeka endapo mienendo ya sasa itaendelea kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana.
Katika taarifa yao ya siku ya kupinga ukeketaji, wakurugenzi wa UNFPA na UNICEF wanasema ukeketaji unachochea ubaguzi dhidi ya wasichana na wanawake na  mwezi Septemba kwenye mkutano wa maendeleo endelevu mataifa 193 yaliafikiana malengo mapya ya kutokomeza ukeketaji ifikapo 2030, hali ambayo imethibitisha kwamba ukeketaji ni janga la kimataifa.
Tarif ahiyo imeongeza kuwa jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuhakikisha lengo hilo linatimia ili kuwalinda na kuokoa maisha ya mamilioni ya wanawake na wasichana.

No comments:

Post a Comment