Babatunde Osotimehin ameyasema hayo akiwa mjini Copenhagen, ambako anahudhuria mkutano wa "Women Deliver" ukiwa ni mkutano wa kwanza mkubwa kujadili masuala ya uzazi , kujamiiana na afya ya uzazi , tangu viongozi wa dunia kupitisha malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs.
Mkutano huo unaangazia jinsi ya kutekeleza malengo hayo ili yawanufaishe wanawake na wasichana. Bwana Osotimehin anaeleza ni kwa nini maendeleo endelevu yanaanza na familia
(SAUTI YA BABATUNDE)
"Ni kuhusu watu, na huwezi kuwa na maendeleo endelevu bila watu, bila ku wapa elimu na fursa ya kuweza kujikimu, na wanawake na wasichana ni kitovu cha maendeleo, kile kinachowafanya kuwa jinsi walivyo ni uwezo wa kuchagua kuhusu masuala ya uzazi. Kuamua lini wanataka kupata watoto na watoto wangani wanawotaka, kwa wasichana , ni kuweza kwenda shule na kusalia huko ili kufikia malengo"
No comments:
Post a Comment