Sunday, 10 April 2016

UZAZI WA MPANGO KWA NJIA YA ASILI


“BILLINGS OVULATION METHOD”

Ili kujifunza njia hii vizuri, ni vyema kuvifahamu vizuri viungo vya uzazi vya mwanamke na jinsi vinavyofanya kazi.

Viungo vya uzazi vya kike:
 • Hypothalamus
 • Glandi ya Pituitary
 • Tumbo la uzazi
 • Ngozi nyororo
 • Mlango wa tumbo la uzazi
 • Uke
 • Mirija miwili
 • Vifuko viwili vya vijiyai
 • Vijifuko vya vijiyai na vijiyai

Msichana anazaliwa na vijiyai vingi, lakini vyote ni vichanga. Wakati wa kubalehe viungo hivi vinaanza kushirikiana na kuwa na mahusiano kama ifuatavyo:-
 1. Sehemu ya ubongo iitwayo Hypothalamus, inaamsha Pituitary Gland                 
kutengeneza chachu mbili:

 (1) Follicle Stimulating Hormone- kazi yake ni kuamsha kijifuko cha kijiyai na kijiyai
        kukua.  

  (2) Luteinising Hormone- kazi yake ni kupasua kijifuko cha kijiyai      
       na kukiondoa kijiyai baada ya kuiva.
  
 1. Wakati wa kukua kijifuko kinatengeneza chachu ya Estrogen.
               Estrogen ina kazi mbili:
 1. Kuamsha ngozi nyororo kukua
 2. Kuamsha vikunjo vya mlango wa tumbo la uzazi vya L, S, P kutengeneza ute wa kuvutika na kuteleza, yaani ute wa uzazi. Wanawake wengine wanaona furaha wakati Estrogen inapofanya kazi.
 3.   
 4. Baada ya muda kijiyai huiva na LH inapasua kijifuko na kukitoa
kijiyai.Hii huitwa Ovulation:- kuchopoka kwa kijiyai.
Kijiyai kinapokelewa katika mrija, kinaishi hapa kwa siku moja tu (masaa 24), na kinakufa hapohapo na kuyeyuka hapohapo.
 1. Mara baada ya Ovulation kijifuko kinabadilisha:-
  1. Kazi yake: Inatengeneza chachu ya Progesterone na kuongeza tena Estrogen.
  2. Jina lake huitwa sasa Corpus Luteum.
  3. Rangi yake: Kuwa manjano na inafanya kazi kwa muda wa siku 11-16.
 
 1. Progesteron ina kazi tano:-
  1. Inasimamisha Pituitary Gland kutengeneza F S H na L H, ili kijiyai kingine kisiive sasa.
  2. Inarefusha mishipa ya damu ya ngozi nyororo na kuikunja, ili binadamu mpya apate chakula na oxygen ya kutosha akizama hapa.
  3. Inapandisha joto la mwili kidogo kiasi cha 0.°C - O.6°C
  4. Inaamsha vikunjo vya chini vya mlango wa tumbo la uzazi kutengeneza ute mzito sana, ute wa (G) ambao haupitishi mbegu za bwana na kufunga mlango wa tumbo la uzazi mpaka hedhi inapoanza au mpaka kuzaa.
  5. Inaamsha “Pockets of Shaw” kutengeneza manganizi kwa kukausha ute wa uzazi.
         Angalizo: Kwa wanawake wengine wanaona moyo mzito kidogo
                          Progesteron inapofanya kazi.

 1. Kama mama hakupata mimba, Corpus Luteum inaacha kazi yake baada ya siku 11-16 na chachu za Estrogen na Progesteron zinapungua. Hapo ngozi nyororo inatoka pamoja na damu na joto la mwili linashuka tena. Hii huitwa hedhi.

MLANGO WA TUMBO LA UZAZI, VIKUNJO VYAKE NA AINA YA UTE

A.      Katika mlango wa tumbo kuna vikunjo mbalimbali-
 • vikunjo vya L, S, na P vinatengeneza ute wa uzazi Estrogen ikizidi.
 • vikunjo vya G vinatengeneza ute usio na uzazi Progesteron ikizidi
 •  
 1. Ute wa G kazi yake ni :-
Kufunga mlango wa tumbo la uzazi. Mbegu za baba na vijidudu vya magonjwa haviwezi kupita. Ute wa G hauna uzazi.
 
 1. Ute wa L kazi yake ni:-
 2.  
 • Kuchuja mbegu dhaifu 400,000,000→200.
 • Kufungia mbegu zenye nguvu katika vikunjo vya S. Ute wa L una uzazi.
 •    
 1. Ute wa S kazi yake ni:-
 • Kulisha mbegu za baba, zinaishi siku 3-5. Katika mazingira yasiyo na uzazi zinakufa kabla ya nusu saa.
 • Ute wa S unaziwezesha mbegu kuingia katika tumbo la uzazi.Ute wa S una uzazi.
 •  
 1. Ute wa P kazi yake ni:-
 • Kuyeyusha ute wa G na kufungua mlango wa tumbo la uzazi.
 • Pamoja na Enzyms wa Z-granula, huyeyusha ute wa L na kufungua vikunjo vya S ili mbegu ziweze kutoka na kuingia katika tumbo la uzazi na kufuata kijiyai.
 • Huzisukuma mbegu ndani.
 • Kuchuja mbegu za baba.Ute wa P una uzazi.
 •  
 1. Ute wa F kazi yake:- Haijulikani.
       

MIANDAMO

1. AINISHOMwandamo ni muda kutoka siku ya kwanza ya hedhi mpaka
    siku ya kwanza ya hedhi inayofuata.

2. Mabadiliko mbalimbali katika mwandamo: damu, ukavu, ute mzito,
    ute wa kuteleza, ukavu tena n.k

3. Aina ya miandamo.
(1) Mwandamo wa wastani, siku 25-34
(2) Mwandamo mfupi, siku 18-24
(3) Mwandamo mrefu, siku 35-50 au zaidi
(4) Mwandamo bila utaratibu.


*Hakuna sababu ya kurekebisha mwandamo, ni maumbile yake.
  Wasitumie dawa ya chachu bandia, zina madhara mengi, pia zinaleta utasa.

SIKU YA KIJIYAI KUCHOPOKA

Umuhimu wa kilele ni kwamba kijiyai kinachopoka hapa, yaani siku ya kilele yenyewe, au siku moja baada ya kilele, au siku ya pili baada ya kilele.

*Kama kawaida kijiyai kimoja tu kinachopoka katika mwandamo mmoja. Lakini inaweza kutokea kwamba vijiyai viwili au vitatu vinachopoka. Lakini vyote vinachopoka siku moja tu, yaani katika masaa 24. Vijiyai vyote vinaishi masaa 24 tu. Hakuna kijiyai kinachoiva tena mpaka mwandamo unaofuata.


DALILI ZA KUCHOPOKA KIJIYAI                        
 1. Kilele.
 2. Mdomo wa uke unavimba upande kijiyai kinapoiva.
 3. Tezi kwenye nyonga inavimba upande kijiyai kinapoiva.


KANUNI ZA KUPUMZIKA KUZAA

 1. Kanuni ya kutogusana
Kuacha tendo la ndoa kabisa wakati wa siku zote za uzazi, yaani:
 • bwana asimwage mbegu nje
 • wala mapajani
 • wala kinenani
 • wala kugusana viungo vya uzazi nje, kwa sababu tone dogo la shahawa linaweza kutoka kabla ya mshushio au mshindo na mbegu zinaweza kuingia katika ute wa uzazi uliopo nje na kuogelea katika mifereji ya ute wa uzazi mpaka ukeni na kusababisha mimba.
 • wala kutumia dawa za majira
 • wala kutumia kondomu siku za uzazi.

 1. Kanuni za mapema
  1. kuacha tendo la ndoa wakati wa hedhi.
  2. kuacha tendo la ndoa wakati wa damu kidogo na siku 3 baadaye.
  3. kuacha tendo la ndoa wakati wa ute wa uzazi na siku 3 badaye.
  4. kufanya tendo la ndoa wakati wa siku zisizo na uzazi, ukavu, ute mzito usiobadilika, aina ya majimaji yasiyobadilika jioni tu, si kesho yake.

?Jioni tu: kwa sababu mama ana hakika kama ana ute wa  uzazi au siyo.

?Si kesho yake: Mama hawezi kutofautisha kama ute ni wa
                            mume tu au kama mwenyewe ameanza pia
                            kupata ute wa uzazi.

 1. Kanuni ya kilele
Kuacha tendo la ndoa siku ya kilele na siku tatu baada ya kilele. Kuanzia siku ya nne baada ya kilele tendo la ndoa linawezekana siku na saa yoyote mpaka mwisho wa mwandamo.


FAIDA ZA KUPUMZIKA/ KUACHA TENDO LA NDOA KWA MUDA

 1. Mke apate nafasi ya kujitambua wakati wa kujifunza BOM.
     Kujichunguza ili kuelewa mtiririko wa Ishara zake za uzazi kwa muda   
     wa wiki 2-4.

 1. Mume apate nafasi ya kujenga afya yake wakati wa kujifunza BOM.

     3.  Utaratibu katika ndoa: Kujishinda kunasaidia Kujitawala, na kunaleta     
ukomavu wa akili, mwili na roho, mume anakuwa mtu mwenye maamuzi ya busara.

 1. Uhusiano kati ya mume na mke unaboreshwa, kwa sababu wanaongea mara kwa mara kuhusu siku ya uzazi na zisizo na uzazi.

 2. Inazidisha heshima, upendo na amani. Baba anamjali mkewe,
           wanaheshimiana, mke hawi chombo cha mume kujifurahisha.
     Wanafurahishana katika umoja wa miili.         
 1. Kunaimarisha ndoa na familia. Kwa sababu kunaamsha mapendo ya dhati ambayo yanapata nafasi ya kuonekana katika matendo mengine. Kama wanandoa wanaonyesha mabadiliko ya uwajibikaji katika maisha yao na hivyo watoto wanaiga mifano bora ya maisha ya wazazi. Wanaonyesha upendo, upendo huu siyo kuufunga katika tendo la ndoa pekee.

 2. Kunaimarisha Jamii na Taifa kwa ujumla. Kwa sababu wanandoa wanakuwa na tabia ya kuwajibika kwa ajili ya mtu mwingine na kushinda ubinafsi katika tendo la ndoa. Kunajionyesha pia hata sehemu za kazi na kwa kiasi kikubwa na chanzo safi cha kushinda tabia ya kuomba na kupokea rushwa na hivyo Taifa linakuwa la watu safi.