Wednesday, 9 March 2016

KWA NINI TUNAAMBIWA WATANZANIA AU WAAFRIKA HATUNA AKILI ???

Mimi kama Mwafrika siyo tu nimelisikia hili ktk kwa watu wasio Waafrika bali nimelishuhudia na ninaelendelea kulishuhidia kila siku kwamba Watu wengi hapa Afrika hatuna akili maana yake ni kwamba hatuwezi kutatua hata vijitatizo vidogo vidogo tu na hii ni kila mahali kuanzia kwenye familia, kazini mpaka kwenye maisha tu ya kila siku!


 1. Nitatoa mifano, ni jambo la kawaida kukuta Mwanaume Mtanzania kanuniana na Mke wake kwa miezi hata mitatu mpaka wazee wasafiri kilometa 800 ktk vijijini kuja kuwafanya waongee, yaani Mwanaume mzima anaamka asubuhi haongei na mke wake anaenda anarudi kimya, ina maana hata kama amesahau kitu nyumbani ambacho ni muhimu hawezi kumpigia mke wake simu labda amuombe amletee au akipeleke mahali kwa kuwa kamnunia lkn ni mtu anayelala naye kitanda kimoja, wanaishi nyumba moja sasa hii ni tabia ya kitoto na ya watu wasiokuwa na akili na mtu anayestahili kuitwa mtu mzima hawezi kufanya hivi!

  Ukija kwenye mambo ya siasa watu siku zote hupoteza muda kujadili mambo ambayo siyo muhimu kwa mfano leo kuna Ugeni wa Raisi ktk Vietnam kwa kawaida jamii ya watu wenye akili wangekuwa wanajadili sababu za ujaji wa raisi hapa nchi lkn kilichotawala majadilliano ni kwa nini Raisi wa nchi hakwenda Uwanja wa ndege kumpokea raisi na watu wanapoteza muda kujadiliana kama amekosea au la, sasa mtu mwenye akili hafanyi hivyo!

  Ukija huku barabarani kama dar es salaam utakuta kitu kidogo kinasababisha foleni ya masaa mawili labda kuna mwanamke tu kavaa nguo inayoonyesha maumbilie yake sasa magari hayaendi na watu wanasimama kuanza kumtukana huku foleni ni kubwa watu wanachelewa na uzalishaji unasimama shauri ya mwanamke mmoja tu!

  Huwezi kuwaambia watu kitu mara moja wakaelewa ni lazima utumie nguvu na ikiwezekana Polisi ndiyo waelewe kwa mfano nilikwenda kwenye mahafali ya kumaliza Chuo Kikuu wakasema Mwanafunzi akiitwa kuja kuchukuwa cheti mmuwaache aje mwenyewe akabidhiwe cheti chake halafu wakati anarudi ndiyo muanze kumpongeza ili kuokoa muda hilo halikuwezekana pmj na kurudiwa kusemwa mara karibia 10 mtu akiitwa watu wanamzingira wanaanza kupiga picha matokeo yake anashindwa kwenda ikabidi Polisi waje ili kulifanikisha hilo!
  sasa watu wenye akili huwa hawafanyi hivyo kwani husikiliza wanachoambiwa na kutekeleza!

  Ukimuuliza mtu kitu hasikilizi halafu anakupa jibu ambalo haujamuuliza mifano iko mingi hata hapa  mtandaoni mtu anasoma kichwa cha habari bila kusoma maudhui ya kilichoandikwa na kuanza kujibu na wkt mwingine kumtukana aliyeleta mada bila hata ya kuelewa kilichaoandikwa, anauliza kile ambacho tayari kimeshaelezewa kwenye mada ambapo alipaswa kusoma tu na kuelewa lkn bado anakuuliza!
  Na mfano mingine mingi sana, sasa ni kwanini lkn hatuna Akili????
  Tunawezaje kuindustrialize na kushindana na Dunia kama hatuwezi kutatua hata vitu vidogo kama hivi?